Thursday, September 20, 2012

ACT TAYO National Youth Conference

From 13th - 17th September we held a national youth conference at St. John's University, Dodoma. Over 500 young people attended together with their leaders and they came from many different areas of the country, representing 21 of the 27 dioceses of the Anglican Church of Tanzania. The conference included teaching from God's Word and on a variety of different subjects affecting the youth of the church in Tanzania. The theme of the conference was "live at peace with everyone" (Romans 12:18) Many of the groups attending were youth choirs and so one day was devoted to a music festival in which each choir sang a song that they had written based on the main theme as well as other songs. We also had sports competitions in football and netball, the Southern zone winning netball and the Coast and Eastern zone winning football.

(Tarehe 13-17 Septemba 2012 tulikuwa na kongamano la vijana la jimbo, lililofanyika katika St. John's University, Dodoma. Zaidi ya vijana 500 pamoja na viongozi wao walihudhuria na walitoka sehemu nyingi za bara na visiwani (Zanzibar), Tanzania, wakiwakilisha dayosisi 21 kati ya madayosisi 27 ya Kanisa Anglikana Tanzania. Katika kongamano hili tulikuwa na mafundisho ya Neno la Mungu na katika mada mbalimbali zinazohusu vijana wa kanisa Tanzania. Neno kuu la kongamano ilikuwa "Mkae katika amani na watu wote (Warumi 12:18) Vikundi vingi vilivyohudhuria vilikuwa vikundi vya kwaya na siku 1 tulikuwa na tamasha la uimbaji. Kila kwaya iliimba wimbo 1 wa neno la kongamano pamoja na nyimbo nyingine. Pia kulikuwa mashindano ya michezo ya mpira wa miguu na mpira wa pete (netball). Kanda ya kusini walikuwa washindi katika mpira wa pete, na kanda ya Pwani na Mashariki katika mpira wa miguu.)

 
TAYO Chairman, Johnson Mgimba, Archbishop of Tanzania, Most Rev. Dr. Valentino Mokiwa, VC St. John's University of Tanzania, Professor Mwaluko, General Secretary, ACT, Rev. Dr. Dickson Chilongani


The conference was opened by the bishop Rt. Rev. Baji and closed by the asrcbishop of Tanzania, Most Rev. Dr. Valentino Mokiwa with the General Secretary of ACT, Rev. Dr. Dickson Chilongani We were also warmly welcomed to the University by the Vice Chancellor, Professor Mwaluko and Professor Kamwaya.
(Kongamano lilifunguliwa na Rt. Rev. Askofu Baji na kufungwa na Askofu Mkuu wa Tanzania, Most Rev. Dr. Valentino Mokiwa, pamoja na Katibu Mkuu, KAT, Rev. Dr. Dickson Chilongani. Pia tulikaribishwa sana katika chuo kikuu na Vice Chancellor, Professor Mwaluko, pamoja na Professor Kamwaya.)


Football Competition
The conference was a great success and was a great opportunity for young Christians from across Tanzania to come together in fellowship. We are very grateful to all those who supported us financially and in prayer to make this event possible. God Bless you.


Preacher Rev. Canon George Chiteto
(Kongamano lilikuwa na mafanikio makubwa sana na ilikuwa nafasi nzuri kwa vijana wa kikristo kutoka sehemu nyingi za Tanzania kushirki kwa pamoja. Tunawashukuru wale wote waliotusaidia kifedha na katika maombi ili kutuwezesha kufanya kongamano. Mungu awabariki sana.)








School of Music and Worship

The whole group with certificates
From August 6th -28th 2012 we held a school of music for young Christian musicians, aimed at encouraging them in their ministry and helping them to increase their musical skills and knoweledge as well as giving them an understanding of the importance of music ministry in the church. The school was held at St. John's University in Dodoma and 25 students attended from 8 different dioceses across the Anglican Church. 
Students practising the guitar






Ev. Musa Njagamba teaching piano
We were also joined by students from different denominations including Lutheran, Pentecostal and Roman Catholic and it was a great blessing to share with such a wide range of people. The course was taught by Meraby Kaimukilwa, from the music school of Ruhija Academy in Bukoba, Tanzania, together with Evangelist Musa Ngajamba, and Youth Development Consultant for ACT, Christine Salaman.

Ev. Musa Njagamba
Subjects taught included music theory, song writing, playing guitar and piano, history of music, using music in church and singing. Each day also included teaching from God's Word, praise and worship. The course was a huge success and of great benefit and blessings to all the students.



(Tarehe 6-28 Agosti 2012 tuliendesha shule ya muziki kwa ajili ya vijana wa kikristo ambao ni wanamuziki, ili kuwatia moyo katika huduma yao na kuwasaidia kuongeza ujuzi na uelewa wao katika muziki pamoja na kuwasaidia kuelewa umuhimu wa huduma ya muziki katika kanisa. Shule hiyo ilifanyika katika St. John's University, Dodoma na wanafunzi 25 walihudhuria kutoka madayosisi 8 ya kanisa Anglikana Tanzania. Pia wanafunzi wengine walitoka madhehebu mbalimbali kwa mfano Kilutheri, Pentekoste na RC na tulibarikiwa sana kushirikiana na watu mbalimbali tofauti. 

Christine Salaman teaching





Meraby Kaimukilwa teaching Guitar

Students in Class
Shule ilifundishwa na Meraby Kaimkilwa wa shule ya muziki, Ruhija Academy, Bukoba, pamoja na Mwinjilisti Musa Njagamba na Mshauri wa Maendeleo ya Vijana, ACT, Christine Salaman. Masomo yaliyofundiwa yalikuwa theory ya muziki, kutunga nyimbo, kucheza gitaa na kinanda, historia ya muziki, ufanisi wa kutumia vyombo katika ibada, na uimbaji. Pia kila siku tulikuwa na mafundisho ya Neno la Mungu na vipindi vya sifa na kuabudu. Shule ilikuwa na mafanikio makubwa na iliwasaidia na kuwabariki sana wanafunzi wote.)
Prize winning students with their teachers














 








Monday, July 30, 2012

TAYO Fundraising Event/ Small Loans Update

Bishop Michael Hafidh of Zanzibar, Guest of honour
 Mh. Otieno Igogo,
General Secretary, ACT, Dr. Dickson chilongani
On 21st July 2012 we held a big fundraising event at the Landmark Hotel, Dar-es-Salaam to support TAYO projects. We thank God that the event went well and are very grateful to our planning committee in Dar who put in a lot of work to make the event a success. Many choirs and solo artists were present and helped make the event into a joyful celebration. The guest of honour was Otieno Igogo, president of the Tanzania tax payers association and we are very grateful to him for his generous donation.
Guest of honour entering with Rev. Johnson Lameck,
Youth Co-ordinator, Dar-es-Salaam
In total we raised around 18 million tanzanian shillings (over £7000). This will mainly go towards supporting our recording studio project. This is a huge step though we are continuing with the fundraising effort as more is still needed. If you are able to support us in this please make a donation on our just giving page on the link above.
Organising Committee
(Tar 21/07/2012 tulifanya tamasha kubwa la uchangiaji katika Landmark Hotel, Dar-es-Salaam kwa ajili ya miradi ya TAYO. Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya tamasha na pia tunawashukuru kamati yetu ya maandalizi kule Dar ambayo ilifanya kazi kubwa ili kufanikisha tamasha hili. Kwaya nyingi pamoja na waimbaji binafsi walikuwepo na walisaidia tamasha liwe la furaha kubwa. Mgeni Rasmi alikuwa Mh. Otieno Igogo, rais wa jumuiya ya walipa kodi, Tanzania, na tunamshukuru sana kwa mchango wake mkubwa.
Jumla ya michango yote ilikuwa TSh. 18,000,000 (zaidi ya £7000). Tutatumia fedha hizo hasa kwa mradi wetu wa kujenga studio ya kurekodi. Hii ni hatua kubwa lakini bado tunaendelea kuchangisha fedha maana bado tunahitaji zaidi. Ukiweza kutusaidia na mchango angalia ukarasa wetu wa "justgiving" kupita link hapo juu.)


Johnson Mgimba
Chairman, TAYO
















Also a few weeks ago we visited the diocese of Mpwapwa to asses the small loans and savings project which is half way through in that diocese. We visited 6 youth groups and their projects which included keeping pigs, chickens and goats, making gravel and selling bibles and other church resources.
All the projects are going well and the groups are successfully returning their loans and making savings. Please pray that their projects will continue to be a success and bring benefits to them, their families and their communities.





(Pia wiki chache zilizopita tulitembelea dayosisi ya Mpwapwa ili kufanya tathmini ya mradi wa kuweka na kukopa ambayo imefika katikati ya muda wake katika dayosisi ile. Tulitemblea vikundi 6 na miradi yao kwa mfano ufugaji wa nguruwe, kuku na mbuzi, kuponda kokoto na uuzaji wa biblia na vitu vingine vya kanisa. Miradi yote inaendelea vizuri na vikundi vinaendelea vizuri katika kurejesha mikopo yao na kuweka akiba.
Tunaomba maombi yenu kwamba miradi yao iendelee kuleta mafanikio na kuwafaidisha wanachama wenyewe, familia zao na jamii zao.)



Tuesday, June 5, 2012

Video of TAYO work 2012

This video shows some of the work of the TAYO youth office during 2012. If you would like a longer version of this video showing more of this work (mostly in Kiswahili) it is available on DVD - please let us know.

(Video hii inaonyesha baadhi ya kazi za ofisi ya vijana, TAYO, 2012. Ukipenda kuona video ndefu zaidi inayoonyesha kazi hizo (kwa sehemu kubwa kwa Kiswahili) inapatikana kwa DVD - utujulishe)


Tuesday, May 22, 2012

TAYO Committe Meeting and National Youth Conference

At the end of April we held our first meeting with the new TAYO committee. We were able to discuss our vision for the future and make plans for the coming years. We also were able to meet with the General Secretary of ACT and discuss the future of TAYO with him. Since this meeting we have developed a new strategic plan for TAYO for the next 3 years. The picture shows the committee together with the General Secretary, ACT and the youth projects officer, ACT at Kemmy Lodge in Dodoma where the meeting was held.

Mwishoni mwa mwezi wa 4 tulifanya kikao cha kwanza cha kamati mpya ya TAYO. Tuliweza kuongelea kuhusu maono yetu na kuweka mipango ya miaka ijao. Pia tulikutana na Katibu Mkuu wa KAT na kujadiliana naye kuhusu TAYO. Baada ya kikao tumeandika Mpango mkakati mpya wa TAYO kwa miaka mitatu ijao. Picha hii inaonyesha kamati tendaji ya TAYO pamoja na Katibu Mkuu, KAT na Afisa Miradi wa Vijana, KAT. Tulifanyia kikao Kemmy Lodge, Dodoma.
This year we are planning a national youth conference which will be held on the 13th -17th September at St. John's University. Young people and youth leaders from every diocese have been invited and we expext to have over 700 participants. The aim of the conference is to encourage the young people and to increase unity. The conference will include bible teaching and teaching in a range of different subjects relevant to young people in Tanzania. There will also be a chance for the youth choirs to sing and praise God and a sports competition. The key bible verse for the conference is Romans 12:18 ".... live at peace with everyone". Please pray for all the preparations for this event and for God's blessings on it.

Mwaka huu tunapanga kufanya Kongamano la Vijana la Jimbo litakalofanyika tarehe 13-17 Septemba katika chuo kikuu cha St. John. Vijana na viongozi wao kutoka kila dayosisi wamealikwa na tunategemea kuwa na wajumbe zaidi ya 700. Lengo la kongamano ni kuwatia moyo vijana na kujenga umoja. Tutakuwa na mafundisho ya neno la Mungu na katika mada mbalimbali zinazohusu vijana wa Tanzania. Pia kutakuwa vipindi vya uimbaji na mashindano ya michezo. Neno kuu la kongamano ni kutoka Warumi 12:18 ".... mkae katika amani na watu wote". Tunaomba maombi yenu katika maandalizi yote na tunaomba baraka za Mungu kwa ajili ya kongamano hilo.

We are currently trying to raise funds for this event. Each participating diocese will contribute but after this we will still have a deficit of around £2,500. We would be grateful for any contribution you are able to make on our just giving page http://justgiving.com/ACT-Youth-projects  Please indicate that your contribution is for the youth conference. The pictures show our youth conference in 2009 which was the last time we were able to put on a national conference

Sasa tunatafuta fedha kwa ajili ya tukio hili. Kila dayosisi itachangia lakini bado tutakuwa na upungufu wa kama TSh. milioni 5. Tutakushukuru sana ukiweza kuchangia kupitia "just giving"  http://justgiving.com/ACT-youth-projects  Ukichangia uonyeshe ni kwa ajili ya kongamano. Picha hizi zinaonyesha kongamano la vijana la mwaka 2009, mara ya mwisho tulipoweza kufanya kongamano la jimbo.

Tuesday, April 3, 2012

Music and Worship Seminar, Songea and TAYO elections

From the 14th - 17th March, 2012 we held our second music, praise and worship seminar, this time in the Southern zone of Tanzania, including 6 dioceses. The seminar was held in Songea in the diocese of Ruvuma, and nearly 40 participants attended. The seminar was aimed at songwriters and leaders of church youth choirs to help them develop their musical and song-writing skills and also to help them develop spiritually and deepen their understanding of the importance of music and choirs in the church and how to use their skills to really worship God in Spirit and Truth.

Tarehe 14-17 Machi 2012 tuliendesha semina ya pili ya muziki, sifa na kuabudu, katika kanda ya kusini ya Tanzania ambapo kuna madayosisi 6. Semina ilifanyika Songea, dayosisi ya Ruvuma na wajumbe karibu na 40 walishiriki. Semina hii ililenga watungaji wa nyimbo na viongozi wa kwaya za vijana za kanisa, kuwasiaidia kuboresha ujuzi wao katika muziki na pia kuwasaidia kukua kiroho na kuelewa zaidi kuhusu umuhimu wa muziki na kwaya kanisani, na jinsi ya kutumia vipaji vyao kumwabudu Mungu katika Roho na kweli.

The seminar was a huge success and a great blessing to all who attended. We are now preparing for a 1 month music school which will take place in Dodoma in August 2012 and well as a further 2 seminars in the remaining 2 zones of Tanzania. The pictures show some of the participants of the seminar and teacher Musa Njagamba, a musician and evangelist from Singida. We were also joined by evangelist Canon David Haj who taught and ministered at the seminar.

Semina hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa sana na wajumbe wote walibarikiwa sana. Sasa tunaandaa shule ya muziki ya mwezi mzima itakayofanyika Dodoma mwezi wa 8, 2012, pamoja na semina 2 katika kanda 2 za Tanzania zilizobaki. Picha hizi zinaonyesha wajumbe wengine pamoja na mwalimu wao, Musa Njagamba ambaye ni mwanamuziki na mwinjilisti kutoka Singida. Pia Mwinjilisti Canon David Haj alikuwepo kufundisha na kuhudumu katika semina.



On the 27th March 2012 we held elections for a new TAYO committee which will lead the organisation for the next 3 years. We are very pleased that a dedicated committee of 8 youth leaders from different dioceses across Tanzania have been elected, led by chairman Mr. Johnson Mgimba of the diocese of Ruaha. We ask for your prayers for them as they begin their work and we pray that the work of TAYO will be strengthened and blessed. We also thank the retiring comittee who have led TAYO for the last 4 years.
Tarehe 27 Machi 2012 tulifanya uchaguzi wa kamati mpya ya TAYO itakayoongoza TAYO kwa miaka 3. Tumefurahi kwamba kamati nzuri ya viongozi wa vijana 8 wa madayosisi mbalimbali ya Tanzania imechaguliwa, ikiongozwa na mwenyekiti Mr. Johnson Mgimba wa dayosisi ya Ruaha. Tunaomba maombi yenu wanapoanza kazi yao na tunaomba kazi ya TAYO ipate nguvu na baraka. Pia tunawashukuru kamati ya zamani ambayo imeongoza TAYO kwa miaka 4 iliyopita.
The elections were led by the Most Rev. Dr. Valentino Mokiwa, archbishop of Tanzania and Rev. Canon Dr. Dickson Chilongani, general secretary of the Anglican Church of Tanzania, and we welcomed a special Guest, the Rt. Rev. Bill Atwood from Nairobi. Delegates attended from 20 of the 26 dioceses of ACT. The pictures show some of the delegates being addressed by the Archbishop, and the new committee receiving his blessing.
Uchaguzi uliongozwa na Most Rev. Dr. Valentino Mokiwa, Askofu Mkuu wa Tanzani, na Rev. Canon Dr. Dickson Chilongani, Katibu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, na pia tulimkaribisha mgeni Rt. Rev. Bill Atwood kutoka Nairobi. Wajumbe walishiriki kutoka madayosisi 20 kati ya madayosisi 26 ya KAT. Picha hizi zinaonyesha baadhi ya wajumbe wakimsikiliza Askofu Mkuu, na kamati mpya ya TAYO wakipokea baraka yake.


The new committee together with members of the retiring committee and ACT  youth officers
In front: TAYO Chairman, Johnson Mgimba; Rt. Rev Bill Atwood, Most Rev Dr. Valentino Mokiwa, Archbishop; Rev Canon Dr. Dickson Chilongani, General Secretary

Monday, February 6, 2012

Small Loans and Recording Studio

We praise God that the small loans and savings project in Mpwapwa diocese is progressing well. We had a 2 day training session in January, initially training the committee who will help us to run the project at the diocese and then training leaders from all the groups who will be developing small projects. 11 groups are participating from the diocese and are developing a variety of projects such as pig and chicken farming, agricultural buisness and vegetable gardening, brick making, selling bibles and prayer books etc.
On 31st January we returned to the diocese to give out the loans which had been agreed. Loans of between 400,000 and 600,000 Tanzanian Shillings were given to each group (around £260-£440) and we have also taught the groups to make their own savings so that their projects will be sustainable in the future. Please pray that the individual projects will develop well and the groups will be able to return their loans on time as well as making a profit. These pictures show the training course in Mpwapwa cathedral, with our project officer, Justine Sabe, teaching.

(Tunamshukuru Mungu kwamba mradi wa kuweka na kukopa katika dayosisi ya Mpwapwa unaendelea vizuri. Tulifanya mafundisho wa siku 2, mwezi wa kwanza, kuanzia na kamati amabyo itatusaidia kuendesaha mradi dayosisini, na halafu mafundisho kwa viongozi wa vikundi vitakavayoshiriki katika mradi. Vikudi 11 vinashiriki, katika dayosisi hiyo na wanaendelea na miradi mbalimbali kwa mfano ufugaji wa nguruwe na kuku, biashara ya kilimo na bustani, kufyatua matofali, uuzaji wa biblia na vitabu vya sala, nk. Tarehe 31 Januari tulirudi Mpwapwa kutoa mikopo. Tulitoa kati ya TSh, 400,000/= na TSh. 600,000/= kwa kila kikundi, na pia tuliwafundisha kuweka akiba za fedha ili miradi itakuwa endelevu. Tunaomba maombi yenu ili miradi ya vikundi iendelee vizuri na vikundi vitaweza kurudisha mikopo kwa wakati pamoja na kupata faida. Picha hizi zinaonyesha mafunzo katika kanisa kuu la Mpwapwa, na Afisa Miradi, Justine Sabe, akifundisha)

We are continuing fundraising for our project to develop a recording studio in Dodoma for youth choirs to use. This project will be a huge benefit to youth choirs who like to record their music to spread their Gospel message and to raise money for their groups. It will also provide a source of income for the youth office. We desperately need more funding for this project. If you are able to make a donation to support this project please donate on the just giving page above. Or if you would like to buy a CD of local choirs, or feel you could sell some of these for us please contact us at TAYO@anglican.or.tz

(Pia tunaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya mradi wetu wa kufungua studio ya kurekodi hapa Dodoma, kwa ajili ya kwaya za vijana. Mradi huu utasaidia sana kwaya za vijana kwa sababu vijana wanapenda kurekodi ili wahubiri injili zaidi na wapate chanzo cha mapato kwa vikundi vyao. Pia studio itasaidia kupata fedha kuendesha ofisi yetu ya vijana. Tunahitaji sana kuongeza fedha katika huu mradi. Ukiweza kuchangia tunaomba mchango wako katika "just giving" hapo juu. Au ukipenda kununua CD za kwaya mbalimbali, au utaweza kutusaidia kuziuza unaweza kuwasiliana nasi kwa email TAYO@anglican.or.tz)